๐๐AFRKA TUAMKE๐ฉ๐ฑ Misri ilikua ni Afrika kwa maandishi yake,utamaduni wake na namna yake ya kufikiri" .Hivi ndivyo anavyohitimisha mtaalamu wa masuala ya kale ya Misri(Egyptologist) raia wa Ufaransa Jean Vercoutter na mpinzani wa Cheikh Anta Diop katika mkutano wa Cairo juu ya utambulisho wa Wamisri wa kale. Mkutano wa Cairo ulifanyika Mwaka 1974,UNESCO taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuamua masuala kama hayo,ilikubali kua Cheikh Anta Diop na Theopile Obenga wako sahihi kua Misri ya kale ilikua ni ustaarabu(Civilazation) wa kiafrika katika nyanja zote,hii ilitokea baada ya malumbano makali kati ya Egyptologist wawili wa Kiafrika na wenzao wawili. USHAHIDI Tofauti na mtu atakavyoelekezwa kuamini,Misri ilikaliwa na watu waliokua wanahamia kutoka Kusini kwenda Kaskazini na watu weusi walioitwa Anu. Hawa ni watu waliotokea Kusini mwa Afrika na maeneo ya maziwa makuu ambao walilowea kwanza...
Machapisho
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
AFRIKA TUAMKE. . ๐MWAFRIKA: ALIZALIWA PARADISO SASA ANAISHI JEHANAMU Afrika ni bara lenye utajiri mwingi, lakini ni bara masikini kuliko yote duniani. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, kati ya nchi 48 masikini sana duniani, 33 zinatoka Afrika, ikiwamo Tanzania. Zaidi ya hilo, Afrika ndilo bara pekee lenye deni kubwa la nje kuliko mabara yote duniani ambapo mpaka sasa deni hilo limefikia dola za Marekani bilioni 980 [ukiondoa riba], na linazidi kuongezeka. Katika deni hili, Tanzania inadaiwa dola bilioni 40, kabla ya riba. Huo ni upande mmoja wa hadithi hii ya kusikitisha. Lakini hebu tujiulize: Je, Afrika imechangia nini katika ustaarabu wa dunia, sayansi na teknolojia?. Bila shaka jibu ni: HAKUNA, licha ya kwamba Afrika ndipo mahali alipoumbwa na kuishi binadamu wa kwanza, maarufu kwa jina la Zinjathropus. Tujiulize tena: Je, Afrika imechangia nini cha maana na cha kukumbukwa, katika nyanja za maendeleo, elimu na utamaduni wa dunia?. Hapa ...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
UHALISIA JUU YA TAIFA LA ISRAEL:::-๐๐wengi wao wanasifia namna hili taifa lilivyo/linavyo endesha shughuli zake za kila siku na namna lilivyoweza kufanikiwa kuhimili mikiki mikiki dhidi ya waarabu tangu kuanzishwa kwake 14 May 1948, Mbaya zaidi wengi wamefikia hata hatua ya kusifia kila linalofanywa na hawa wanaojiita wayahudi wakidhani ni lazma kibiblia kufanya hivyo,kama ukiwa na moyo wa Mungu ndani yako unatakiwa uwaonee sana huruma Wapalestina wanaouliwa kinyama na hawa wayahudi huko Gaza na sehemu zingine duniani,kama una Roho ya Mungu ndani yako ulitakiwa usiku na mchana ulie na kuomboleza na kuwaombea raia wa Syria,Iraq,Jordan wanaokufa maelfu na maelfu kila kukicha baada ya kuchonganishwa na hawa wanaojiita wayahudi! kama kweli una roho ya Mungu ndani yako ulipaswa kuhuzunika sana juu ya watu wa DRC CONGO,SOMALIA,SOUTH SUDANI,AFGHANISTAN ambao hawaijui amani tangia kuanzishwa kwa mataifa yao! Kumbuka kuwa Yesu alikufa pale msalabani kwaajili yao pia,na wapo miongoni mwao...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
๐ ๐บ๐ฒ๐ฒ Mnyama-Mwitu pv Mwenye Vichwa Saba Anayetajwa Kwenye Ufunuo Sura ya 13 Anawakilisha Nini?๐๐ฒ Jibu la Biblia ๐๐ Mnyama-mwitu mwenye vichwa saba anayetajwa kwa mara ya kwanza katika Ufunuo 13:1 anawakilisha mfumo wa kisiasa wa ulimwenguni pote. Mnyama-mwitu huyo ana mamlaka, nguvu, na kiti cha ufalme, kuonyesha kwamba ana uwezo wa kisiasa.—Ufunuo 13:2. Ana mamlaka juu ya “kila kabila na watu na lugha na taifa,” na kwa hiyo hawezi kuwakilisha tu serikali ya nchi moja tu.—Ufunuo 13:7. Mnyama-mwitu huyo ana sehemu zinazofanana na zile za wale wanyama wanne wanaofafanuliwa kwenye Danieli 7:2-8. Kwa mfano, anatajwa kuwa na sura ya chui, miguu ya dubu, kinywa cha simba, na pembe kumi. Wanyama wanaotajwa katika unabii wa Danieli wanawakilisha wafalme hususa, au falme za kisiasa, zinazotawala kwa kufuatana juu ya milki tofauti-tofauti. (Danieli 7:17, 23) Kwa hiyo, mnyama-mwitu anayetajwa katika Ufunuo sura ya 13 anawakilisha tengenezo lote la kisiasa. ...