Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2017
SOMO: "UBORA WA YESU KRISTO DHIDI YA MTUME MUHAMMAD S.A.W" Katika hili somo sikusudii kutoa kashifa, dhihaka, wala kejeli dhidi ya kiongozi wa imani ya Kiislamu Muhammad (s.a.w) bali kitu ambacho nitakifanya nikutumia maandiko yaliyo andikwa na kukubalika kwenye Imani hizi mbili, Imani ya Kikristo, na imani ya Kiislamu. Baadhi ya rafiki zangu wa kiislamu wamekuwa ni mahodari wa kutushawishi sisi tunaomfuata YESU, tumwache Yesu, na kumfuata Muhammad, kwa madai ya kuwa, yeye ndiye Mwisho wa Mitume. ( مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَٰكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ) الأحزاب (40) Al-Ahzaab Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. Kupitia aya hii Waislamu wamekuwa na imani kuwa, Muhammad yeye ni nabii na mtume wa Mwisho, kwa hivyo Yesu yeye hawezi kuendelea tena kuwa mtawala, na wakazidi kuamini...