SOMO: "UBORA WA YESU KRISTO DHIDI YA MTUME MUHAMMAD S.A.W"
Katika hili somo sikusudii kutoa kashifa, dhihaka, wala kejeli dhidi ya kiongozi wa imani ya Kiislamu Muhammad (s.a.w) bali kitu ambacho nitakifanya nikutumia maandiko yaliyo andikwa na kukubalika kwenye Imani hizi mbili, Imani ya Kikristo, na imani ya Kiislamu.
Baadhi ya rafiki zangu wa kiislamu wamekuwa ni mahodari wa kutushawishi sisi tunaomfuata YESU, tumwache Yesu, na kumfuata Muhammad, kwa madai ya kuwa, yeye ndiye Mwisho wa Mitume.
( مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَٰكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا )
الأحزاب (40) Al-Ahzaab
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Kupitia aya hii Waislamu wamekuwa na imani kuwa, Muhammad yeye ni nabii na mtume wa Mwisho, kwa hivyo Yesu yeye hawezi kuendelea tena kuwa mtawala, na wakazidi kuaminishwa kuwa Muhammad ni Mtume kwa ajili ya watu wote.
( قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ )
الأعراف (158) Al-A'raaf
Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anaye huisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.
Hivyo basi kwa uchache huu wa maandiko ukawaaminisha kuwa, Yesu wakati wake umekwisha kupitia, hivyo Muhammad yeye anabaki kuwa Kiongozi mpaka mwisho wa DUNIA! wapo wanaosema Yesu yeye alikuwa maalum kwa Waisrael tu.
Mathayo 15:24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Matendo 13:23 Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi;
Kitu ambacho kimewaponza wengi hata kuthubutu kumwacha Yesu, ni hayo maandiko ambayo nimeyanukuu kuwa Yesu ametumwa kwa Waisrael, na Muhammad ni mtume wa watu wote, Kitu ambacho kimewafanya wapotee kwa kutokuyajua maandiko.
Mathayo 22:29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
Kitu ambacho Wameshindwa kuelewa, juu ya Yesu kusema kuwa ametumwa kwa Waisraeli, haikuwa na maana kuwa, ni Israel tu, bali Yesu alianza kwanza kwa Wana wa Israel, ili baada ya Kifo chake awavute na wengine wasiokuwa Waisrael waje kwake.
Yohana 12:32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
Kifo cha Yesu kimekuwa ni kiunganishi baina ya Wayahudi na wasiokuwa Wayahudi, Injili imepata kibali cha kuwafikia Mataifa.
Luka 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Kwa hivyo Yesu akatoa kibali kwa Injili yake ihubiriwe kwa Mataifa yote.
Mathayo 28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
"TUJE SASA KWENYE MAIN POINT"
Ubora wa Yesu dhidi ya Muhammad, upo kwenye Majukumu na kazi ambazo amezifanya! kwa sababu Waislamu wanaamini kuwa Yesu ni Mtume na Nabii na Muhammad ni Nabii, nitazungumza katika huo unabii na Utume, kwanza kabisa nianze kumuonyesha Yesu kuwa yeye Utawala wake hauchukuliwi na mtu awaye yote kabla DUNIA haijafika Ukingoni. 👇
Luka 1:31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake
utakuwa hauna mwisho.
Ufalme wa Yesu tunaambiwa hautakuwa na mwisho, Yesu yeye ndiye wa mwanzo na mwisho.
Ufunuo 1:17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho.
Yesu Kristo yeye ni Mtawala na ufalme wake hauwezi kubatilishwa na Muhammad kwa sababu Yesu yeye anasema👇
Luka 10:22 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Mathayo 28:18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yesu amekabidhiwa yote na Baba yake, na Amepewa Mamlaka yote Mbinguni na duniani, Lakini Muhammad yeye anasema👇
( قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ )
الأعراف (188) Al-A'raaf
Sema: Sina mamlaka ya kujipa nafuu wala kujiondolea madhara, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu ningejizidishia mema mengi, wala ovu lisinge nigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa watu wanao amini.
Yesu yeye anayo mamlaka yote ya Mbinguni na Duniani, Lakini Muhammad yeye hata mamlaka dhidi yake yeye mwenyewe hana, unaweza kumweka kwenye mzani pamoja na YESU mwenye mamlaka yote mbinguni na DUNIANI?
"YESU YEYE NI NURU YA ULIMWENGU AMFUATE HAENDI GIZANI"
Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Na pia Ukimwamini Yeye ukifa utakuwa unaishi.
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Lakini MUHAMMAD yeye hajui kitu atakachofanywa yeye wala watakachofanyiwa wale wanaomfuata 👇
( قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ )
الأحقاف (9) Al-Ahqaf
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.
Na Isitoshe yeye atakufa na wanaomfuata Watakufa vile vile kama yeye. 👇
( قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ )
الطور (31) At-Tur
Sema: ngojeni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika wangojeao. (Sifi mimi peke yangu, na ninyi mtakufa Vile vile)
Sasa mwenyewe Fikiria, Ukimfuata Yesu, wewe huendi gizani, bali unakuwa na Nuru ya UZIMA, na ukifa unakuwa unaishi pamoja na KRISTO, yaani unaendelea kuwa na Uhai, lakini ukimfuata Muhammad wewe unakuwa mfu, sawa na Muhammad ni KIPI BORA??? au ni yupi Bora?
Muhammad kafa mpaka LEO hajafufuka, Yesu leo yu hai.
Ufunuo 1:18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Yesu Kristo yu hai Muhammad yeye amekufa, maandiko yanasema juu ya walio hai na Wafu 👇
Mhubiri 9:4 Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);
5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Mwenyewe Soma na upime ni nani Bora zaidi?
YESU YEYE ALIWEZA KUMSIKILIZISHA SAUTI MAITI KABURINI. 👇
Yohana 11:43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
LAKINI MUHAMMAD YEYE HAKUWA NA UWEZO HUO 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
فاطر (22) Faatir
Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
YESU ANAO UHAKIKA WA KUWAPA KONDOO ZAKE UZIMA WA MILELE 👇
Yohana 10:27 Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
28 Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
MUHAMMAD YEYE HANA UHAKIKA WA KUINGIA PEPONI YEYE NA WAFUASI WAKE.
Hadithi ya Aisha kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Fanyeni yaliyo sahihi na yatekelezeni, na furahini kwa kuwa hakuna yeyote atakayeingiziwa peponi kwa amali (matendo) yake” Wakauliza ‘hata wewe mtume wa Allah?’ Mtume (s.a.w) akasema, ‘Hata mimi isipokuwa kama Allah atanifunika kwa rehema zake” (Bukhari Hadihthi Na. 474, Juzuu ya 9)
Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema, Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, “Hakuna yeyote miongoni mwenu atayeokolewa na amali yake” Wakasema hata wewe mtume wa Allah? Mtume (S.A.W) akasema, “Wala mimi isipokuwa anifunike Allah kwa rehema zake; hivyo fanyeni amali njema kwa uadilifu” (Bukhari Hadithi Na. 470, Juzuu ya 9)
TAFAKARI KWA KINA KWA KUUSOMA UJUMBE HUU VEMA KISHA FANYA MAAMUZI SAHIHI.

Maoni
Chapisha Maoni