π πΊπ²π² Mnyama-Mwitu pv Mwenye Vichwa Saba Anayetajwa Kwenye Ufunuo Sura ya 13 Anawakilisha Nini?ππ² Jibu la Biblia ππ Mnyama-mwitu mwenye vichwa saba anayetajwa kwa mara ya kwanza katika Ufunuo 13:1 anawakilisha mfumo wa kisiasa wa ulimwenguni pote. Mnyama-mwitu huyo ana mamlaka, nguvu, na kiti cha ufalme, kuonyesha kwamba ana uwezo wa kisiasa.—Ufunuo 13:2. Ana mamlaka juu ya “kila kabila na watu na lugha na taifa,” na kwa hiyo hawezi kuwakilisha tu serikali ya nchi moja tu.—Ufunuo 13:7. Mnyama-mwitu huyo ana sehemu zinazofanana na zile za wale wanyama wanne wanaofafanuliwa kwenye Danieli 7:2-8. Kwa mfano, anatajwa kuwa na sura ya chui, miguu ya dubu, kinywa cha simba, na pembe kumi. Wanyama wanaotajwa katika unabii wa Danieli wanawakilisha wafalme hususa, au falme za kisiasa, zinazotawala kwa kufuatana juu ya milki tofauti-tofauti. (Danieli 7:17, 23) Kwa hiyo, mnyama-mwitu anayetajwa katika Ufunuo sura ya 13 anawakilisha tengenezo lote la kisiasa. ...
Machapisho maarufu kutoka blogu hii
ULAJI WA APPLE(TUFAA)HUKUWEKA MBALI NA DAKTARI,,,FAHAMU FAIDA ZA KE KIAFYA.π MATUFAA KWA AFYA,LISHE NA TIBA "An apple a day will keep the doctor away…An apple before bed makes the doctor beg his bread" (kula tunda moja la tufaa kila siku humfanya mtu asiwe na haja ya kuonana na daktari…kula tunda la tufaa kila siku humkosesha daktari mapato yake). Misemo hii ya Waingereza inaonyesha umuhimu wa matunda ya matufaa kwa ajili ya kudumisha afya ya binadamu, kukinga na kutibu magonjwa mbalimbali. Matufaa yana Vitamini K, nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals) aina ya quercetin flavonoid. Faida za kiafya Matufaa ni tiba nzuri ya ugonjwa wa kuharisha. Husaidia katika matibabu ya uvimbejoto wa utumbo (colitis) Husaidia katika matibabu na kuzuia shinikizo la damu Husaidia katika tiba na kuzuia magonjwa ya mzio (allergy) pamoja na pumu ya mapafu. Hutibu tatizo la kupata choo kikavu au kutokupata choo (constipation) Ni dawa nzuri san...
Maoni
Chapisha Maoni